Pages

Tuesday, February 28, 2017

ELEWA MAANA PANA YA UJASIRIAMALI

Image result for ujasiriamali

MAANA YA UJASIRIAMALI

Nini maana ya Ujasiriamali?.

Dhana ya Ujasiriamali ina maana pana , miongoni mwa hizo ni;  Mjasiriamali ni mtu ambaye ana hamasa kubwa ya kuleta mabadiliko chanya  katika hali yake ya kiuchumi ambaye ana tabia za kipekee ili kufanikisha azma yake hiyo kwa kujishuhulisha (yaani kujiajiri) ili awe na hali nzuri zaidi kiuchumi.

Pia katika hali nyingine   Mjasiriamali  anaweza kuwa mtu yoyote ambaye anajishughulisha mwenyewe(amejiajiri) katika sekta fulani mfano: kilimo, ufugaji au biashara.

Neno Ujasiriamali lina asili ya Kifaransa " Entreprendre" sawa na Kutekeleza/Kufanya shughuli fulani mwenyewe katika uwanja wa kibiashara katika maana rahisi ni sawa na kuanzisha biashara/shughuli ya kujiajiri.

Kwa mitazamo mbalimbali ya wasomi wana muelezea  Mjasiriamali kama mtu ANAYEONGOZA, ANAYEPANGA na ALIYE NA UTAYARI juu ya hatari zozote zinazoweza kujitokeza katika biashara/shughuli yake husika.  

Mchumi wa KiAustrian  Joseph Schumpeter  ameielezea dhana ya ujasiriamali kwa kuegemea mihimili ya UGUNDUZI na UBUNIFU, katika nyanja hizi(yaani kugundua na kubuni):-
-Bidhaa Mpya
-Njia Mpya za uzalishaji/uendeshaji.
-Masoko Mapya
-Mifumo mipya ya Vikundi na Mashirikisho

UTAJIRI unapatikana pindi UGUNDUZI unapoenda sambamba na MAHITAJI, kwa mtazamo huu tunaweza kusema ya kwamba kazi ya Mjasiriamali ni sawa na kuunganisha mbegu za vigezo fulani katika hali ya Ugunduzi na Ubunifu ili kutengeneza ubora na thamani kwa mteja kwa imani ya kwamba thamani itakayopatikana itafidia gharama za mbegu hizo, na hatimaye kutengeneza faida ya kutosha inayopelekea UTAJIRI.

Mpaka hapa tumeweza kumfahamu huyu Mjasiriamali kwa maana na Mitazamo michache. Je kila Mfanya biashara ndogo ndogo ni Mjasiriamali? Tathmini hili kabla hujasoma Article nyingine!

Shukrani kwa kuwa pamoja.

No comments:
Write comments

Recommended Posts × +