Pages

Friday, April 7, 2017

Je! Unataka Kuiteka Akili Ya Mwanamke. Ni Simple tu.. Mfanyie Vitu Hivi Uone.


Je uko tayari kufahamu jinsi ya kuingia katika akili ya mwanamke na kufanya mapinduzi ya njia ya kawaida unayotumia kuapproach mwanamke? Kama jawabu lako ni ndio, basi zama nami kusoma hizi mbinu ambazo zimethibitishwa kufanya kazi.

1. Anza approach ya mbali

Kabla ya kumuapproach mwanamke, hakikisha ya kuwa unamsoma kwa umbali mambo anayofanya kwanza. Halafu ukiona kama umepata kile unachoweza kutumia kutoka kwake unaweza kumuaproach. Ukiwa unaongea nayeye mwambie kuwa una uwezo wa kusoma nyota yake. 

Wanawake wengi watakubaliana na hili ili kuona ucheshi wako. Halafu ukirudilia na vitu ambavyo ulimsoma awali, utakuwa umemfunga. Mwanzo kama umejaribu kumtabiria vitu ambavyo viko sawa kwake ama vinahusiana na yeye, una nafasi kuu ya kumfanya kukutaka kukufahamu zaidi. Pia ni vizuri kufahamu miondoko ya wanawake na mapema ili kuelewa kama anakubaliana na utabiri wako kwake. 

Pia unaweza kuwambia unaweza kusoma nyota yake kupitia kwa maganja yake. Hii itakupa nafasi ya rahisi kuweza kupata kumgusa bila kukushuku ajenda yako nzima iliyo akilini mwako. Mbinu hii itamfanya yeye kuvutiwa na wewe kwa urahisi.

2. Leta shangwe

Wanawake wanapenda wanaume ambao hawayachukulii maisha serious vile, so hakikisha kuwa unajua jinsi ya kuchat na wanawake.  Unaweza kutumia mbinu ya kutumia kuwa mcheshi na kutoa mizaha ukiwa kando yake. Kufanya hivi kutamfanya yeye kucheka na kutabasamu, jambo ambalo automatic litamfanya yeye kuvutiwa na wewe. Usitumie mbinu ya kumtesa sana na mizaha yako ama utaonekana kuwa na utoto mwingi ama anaweza kukasirishwa. Uzuri wa kutumia ucheshi ni kuwa kunamfanya mwanamke kujihisi bado ana ujana.

3. Ichokore akili yake

Hii ni mbinu ya sanaa ya kutongoza ambayo itamfanya mwanamke yeyote kuathirika kihisia na wewe. Itamfanya akutamani na kuifanya akili kukufikiria wewe tu.

Njia moja kama hii ni kumfanya mwanamke kuingiwa na furaha dakika moja na kukasirika dakika ya pili. Wanawake inaonekana mara nyingi hupenda vioja katika maisha yao, kama vile katika vipindi vya tamthilia ama soap opera. Hoja ya vioja ni nzuri pia kwa kuwa inatoa ile dhana ya kubandikwa jina kuwa unaboa.

Kama unaweza kuyafanya maisha yako kuwa na vioja vya mara kwa mara wanawake watakupenda automatically bila wao kujifahamu. Ukishafanikiwa kuteka hisia zao, inakuwa rahisi kwako kuingia katika akili yao. Unafaa kuonywa ya kuwa kutumia mbinu hii sana inaweza kuwafanya baadhi ya wanawake kuchunguza maisha yako wakitaka kuwa karibu yako kila wakati.

Pia fahamu ya kuwa usimchangaye akili kihisia mwanamke yeyote kwa kutumia mbinu hii kwani mwishowe inaweza kukujeukia.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Wednesday, March 29, 2017

Unataka Mwanamke Apagawe Sana Kwako..!! Basi Tumia Njia Hizi.

Kuna vitu vingi ambavyo unaweza kutumia kwa manufaa yako ili kufanya wanawake wakuone unavutia. Amini usiamini, hivi vitu si lazima uwe tajiri wala uwe na urembo wowote. Mwanzo kati ya vitu hivyo vingi ni rahisi kuvitumia kwa urahisi. Hii hapa ni orodha ya mambo ambayo ukiyazingatia yatakufanya wewe uwe na mnato kwa mwanamke yeyote yule.

1. Uwezo wako wa nishati
Nishati inaweza kuwa na mkusanyiko wa vitu kadhaa, kama vile kuhisi kwa vipepeo ndani ya tumbo, kusuka, wasiwasi ama vitu tofauti kabisa. Kwa mtizamo wa moja kwa moja, nishati inahusiana na yote yale ambayo yanamfanya mwanamke kujiskia raha wakati anapokuona ama kutaka kuutumia muda wake mwingi akiwa na wewe. Nishati inacheza nafasi kubwa katika mapenzi kama wataka kumtongoza mwanamke na ufaulu kwa urahisi. Ili kupeana nishati zaidi kila wakati unapokuwa na mwanamke, hakikisha kile kikuu unachohitaji kufanya ni kumchekesha, kumsapraiz, umguse kwa bahati mbaya mara kwa mara, kuwa mwenye michezo nk. Zote hizo zitamfanya kukufikiria wewe mara 24/7.

2. Mbinu utakayoitumia kumsifu
Kulingana na utafiti kutoka NBC unadai ya kwamba wanawake wengi hawajiskii huru kupewa ama kupokea sifa kutoka kwa wanaume. Lakini usikatwe na tamaa! Vile ambavyo utampongeza mwanamke inaweza kucheza pakubwa kufaulu kumpata mwanamke unayempendae baada ya muda. Afterall ukimsifu kitofauti tofauti anaweza kukubali ama kukuona kama wewe ni mzaha kwake. So kuhepa aibu kama hizi ndogo ndogo, unafaa umsifu mwanamke kwa jambo ambalo ni la kwake pekee, yaani kitu ambacho utamsifu nacho hakipatikani kwa mwingine. Mfano waweza kumakinika kwa kitu ambacho anafanya wakati flani na utumie ujuzi wako wa kiume kumsifia na jambo hilo. Mfano unaweza kumsifu kwa uwezo wake wa kuimba, kuchora, mtindo wake wa kutembea nk. [Soma: Mbinu ya kutongoza kwa wale wanaojifunza]

3. Upambo wako
Si lazima uwe mwanamume wa kuvutia ili umvutie mwanamke. Utafiti umebainisha kuwa wanawake hawavutiwi na urembo wa mwanamume, nywele zake wala ngozi yake. Mwanzo kuwa mrembo kama mwanamume kuna ubaya wake mwingi ikizingatiwa kuwa unaweza kuonekana kama pleya ambaye unapendwa na wanawake wengi.

Kile ambacho unachohitajika hapa ni uhakikishe kuwa uwe nadhifu kimwili na mavazi yako. Kufanya hivi kutakusaidia wewe kuonekana mtu timamu halikadhalika inakufanya wewe kuwa na confidence ya kapproach demu yeyote yule.

4. Ujuzi wako wa kutangamana
Lazima atleast uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kuweza kutangamana na wengine. Kama mwanamume lazima uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kutangamana na wengine kwa urahisi. Hii inamaanisha kuwa lazima uwe na ujuzi flani wa kuongea na wanawake ndipo utakapojua jinsi ya kumfanya apagawe na wewe.

5. Kiwango chako cha kujiamini
Kitu cha mwisho ambacho ni muhimu kwako kuwa nacho ni kujiamini. Kujiamini ni njia moja wapo ya lazima uwe nayo ili uweze kuiteka hisia ya mwanamke yeyote yule.[Soma: Njia za kuwa na confidence kama mwanaume]

KUMBUKA: Vitu vyote tulivyoeleza hapo juu havitakuwa na manufaa yeyote yale iwapo kama hutaweza kujiamini kama mwanamume. Hivyo ni lazima kwako kuhakikisha kuwa mwanzo unajijenga kwa kuwa na confidence. Hii ni kuanzia kujitambua wewe mwenyewe bila kujishuku, kuongea bila woga wowote wala kutoingiwa na wasiwasi wakati wowote ukiwa karibu na mwanamke.

Kama Unashindwa Kumuacha Mpenzi Wako Lakini Unashindwa.Hii Mada Itakusaidia

Kuna watu wana Mikwara sana, ukiachana nae anaanza Maneno ya shombo, wengine hudiriki kukwambia ''you cant live without me utarudi tu'', unajiuliza huyu mtu ana Hisa kwenye mishipa yangu ya moyo au ana mrija wa Oxygen yangu ya kutumia kesho?? Kama nilizaliwa peke yangu kwanini nisiweze kuishi wewe ukiondoka??

Maneno ya mkosaji haya, usiyasikilize kamwe! Unapoamua kufanya Maamuzi magumu usisikilize kingine chochote, Follow your heart. Wengi wamegeuzwa watumwa kwa kuamini they cant live bila watu fulani, kisa wamezoeana, au wamekaa muda mrefu kwenye mahusiano, unahisi kama hutaweza... Hamna kitu kisichowezekana, Mungu ameumba kusahau, utapona maumivu na utasonga! Hakuna destiny rahisi ya Kimapenzi bila kufanya maamuzi magumu, lasivyo Jiandae kuwa mtumwa wa mtu fulani, binadamu fulani ambaye naye amegundua wewe ni dhaifu na anatumia udhaifu wako kukutesa maisha yote...

Amua leo, Uwe mtumwa wa mtu au utengeneze furaha yako kwa Kumove on kupata Lover of you life

Huyu Dada Anaomba Ushauri..Mpenzi Wake Anamuomba Mchezo Ambao Sio.


Kupenda ni ugonjwa na nimeamini kwa kweli huyu jamaa nampenda mpaka nikimwona tuu huwa nasikia kuloa kabla hata hatujaanza, kiukweli nimetoka na others Boy but sijawahi kutana na boy nikampenda hivi na yote ni alivyojaliwa na anavyojua mamboz huwa nafika kunako mlima Kilimanjaro hata mara 4 mfululizo. Ila inanijia mpaka nawaza sijui si ridhiki yangu maana kuna siku tulikua katikati ya mambozi akaanza kunigusa sehemu ambayo siyo kwa kidole nilikua mkali kama chui but alinibembeleza yakaisha.

Juzi tena akajifanya kakosea nilichukia sana leo na kaubaridi hichi nimemcal na kumweleza nipo hostel nahisi baridi nahitaji joto alichonijibu sina hamu eti nambania white. Na ndiyo starehe yake so nampenda huyu Boy jamani naumia maana nasikia tu ukimpa tu mwanaume dharau huanza na kama mwanaume anakupenda kweli hawezi omba huo mchezo.

Nipo dailema jamani nimfanyeje huyu nisimkose? -

Hizi Ndio Sababu Zinazopelekea Wanaume Wengi Wasiwe na Mpango Wa Kuoa


Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa jamii kwamba imekuaje vijana wa kiume wamekuwa ni waongo sana hasa linapokuja swala la kuoa? Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo idadi ya wanaume wanaoogopa kuoa inazidi kuongezeka. Utakuta wapenzi wanaambiana kwamba wanapendana na kuahidiana kuwa wataoana, lakini kitakachotokea baada ya hapo ni mwanaume kuanza kupiga chenga kwa visingizio lukuki.

Kwa nini hali hiyo hutokea? 

Ukweli ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja juu ya tatizo hilo, lakini yapo mambo ambayo yanaweza kutupa angalau tafakuri. Nitajaribu kudadavua baadhi ya sababu zinazowafanya wanaume siku hizi kukwepa kuingia katika taasisi ya ndoa: 

1 Ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano:
Hapa nawazungumzia wale watoto wa kiume waliolelewa malezi ya upande mmoja yaani walilelewa na mama peke yao. Sina maana ya kudharau au kutweza malezi ya mama, la hasha, lakini ni vyema mkafahamu kwamba kuwa na baba asiye na malezi mazuri si sawa na kutokuwa na baba. Na ndio maana nikasema ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano. Achilia mbali aina ya malezi atakayoyapata kwa familia yawe mazuri au mabaya lakini lazima kutakuwa na tabia za kiume zitakazoakisi malezi ya mtoto wa kiume katika familia husika. Watoto waliolelewa na mama peke yao kuna kitu huwa wanakosa, kwani wanakuwa hawana mtu wa kumchukulia kama mfano kwa upande wa jinsia ya kiume na hapo ndipo hujikuta wakijifunza wenyewe namna ya kuongea na kutenda kama wanaume kwa sababu katika makuzi yao hawakupata fursa ya kuwa karibu na baba zao. Kwa kuwa siku hizi kuna kundi kubwa la kina mama ambao wamejikuta wakiachiwa mzigo wa malezi ya watoto, baada ya aidha kuachwa na waume zao au kuzalishwa na kutelekezwa (Single mothers), na hapo ndipo tunaposhuhudia mtoto wa kiume anapokua kwa umri na kimo huku akiwa hana mtu wa kumuangalia kama mfano wa mume anavyotakiwa kuwa katika familia zaidi ya kujifunza mambo hayo kupitia katika TV, senema au miziki. Wanaume waliopitia malezi ya aina hii huchelewa sana kuoa kwani huyaangalia maisha ya ndoa kwa namna ya kujaribu na ndipo hapo wengi huishia kuishi kinyumba na wanawake kwa ajili ya kutaka kujifunza namna ya maisha ya ndoa yanavyotakiwa kuwa na ndio sababu huchukua muda mrefu kufanya maamuzi. Na mara nyingi huishia kubadilisha wanawake kutokana na kutokuwa na uhakika wa kile wanachokitafuta.

2 Mgogoro wa kiuchumi:
Kuna kundi kubwa la vijana siku hizi hawana ajira au hawana uhakika na kipato. Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume atakayependa kujiingiza kwenye ndoa wakati hana kazi au hana uhakika na kipato chake. Na hiyo ni kutokana na wanawake wengi siku hizi kuonekana kujali zaidi wanaume wenye uhakika na kipato. Hii misemo ya wanawake ya kebehi dhidi ya wanaume wasio na ajira au kipato, kama vile “mwanaume suruale” ina mchango mkubwa sana katika kuwafanya wanaume kukwepa kuoa iwapo hawana ajira au hawana uhakika na kipato chao.


3 Wanawake wengi kuwa na kiwango cha elimu ya juu:
Siku hizi wanawake wengi wameibuka katika kutafuta elimu ya juu kwa juhudi kubwa. Idadi ya wanawake wanaojiunga na vyuo vikuu ni wengi tofauti na ilivyokuwa zamani. Na hiyo ni kutokana na wazazi wengi kubadili mtazamo wao juu ya mtoto wa kike. Zamani mtoto wa kike alichukuliwa kama kitega uchumi. Kwa maeneo ya vijijini na katika familia masikini, watoto wa kike walikuwa wanatazamwa kama, ‘biashara ya kesho’ ambapo watauzwa kwa njia ya mahari. Kwa hiyo thamani yao ilikuwa ni kuolewa, ni ile ya kibidhaa na sio kibinadamu. Lakini tofauti na zamani siku hizi hata kule vijijini kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa kumsomesha mtoto wa kike hadi elimu ya juu. Kutokana na mwamko huo wanawake wengi wamejikuta wakiona elimu kama kimbilio pekee la kuepukana na mfumo dume. Mwanamke gani atakubali kunyanyaswa na mwanaume akiwa na elimu yake na labda pia akiwa na kazi yake yenye mshahara na marupurupu ya kutosha, naamini watakuwa ni wachache sana ambao hawajiamini au waliathiriwa na malezi. Kwa upande wa wanaume nao, wamejikuta wakiwaogopa wanawake hawa wenye elimu ya juu kwa hofu ya kuzidiwa kipato na labda kukosa sauti kama mwanaume na hiyo inatokana na ego tu.

4 Wanaume huwaona wanawake kama tishio wanapokuwa na mafanikio makubwa kifedha:
Inaweza kutokea mwanaume anaweza kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye labda tu nisema ni mbangaizaji. Wakati huo anaweza kuahidi kufunga ndoa na mwanamke huyo, lakini iwapo itatokea mwanamke huyo akapata mafanikio kibiashara na kuinuka kifedha. Kama mwanamke asipokuwa makini anaweza kusababisha mwanaume huyo akaingia mitini. Sababu kubwa hapo inaweza kuwa ni hofu ya kuogopa kuongozwa na mwanamke. Kumbuka kwamba mfumo dume bado umetawala vichwani mwa wanaume wengi kutokana na malezi. Mwanaume asiyejiamini ni vigumu sana kwake kuoa mwanamke aliyemzidi kipato. Kwa sababu akifanyiwa jambo dogo tu, inakuwa kama ametoneshwa. Atahisi kutaka kutawaliwa na mwanamke huyo. Jambo ambalo wanawake wanatakiwa kulifahamu ni kwamba kila mwanaume anataka kutambuliwa na kuheshimiwa kama shujaa kabla ya kumfuata msichana. Iwapo utakuwa umesimama iwe ni kifedha au kielimu pale unapotafuta kupata mwenza, inabidi ujishushe sana la sivyo utadoda.


5 Wanaume wengi siku hizi wana hofu ya majukumu, hasa ya kulea watoto:
Kutokana na malezi yao au kile wanachokijua kuhusu watoto, baadhi ya vijana huamini kwamba, kulea watoto ni jambo gumu sana. Lakini wengine wanaamini kwamba, hata mke anapaswa kulelewa kama ilivyo kwa mtoto. Hivyo wanaamua kutafuta kwanza uwezo ambao haupatikani kiurahisi. Kuna wengine, ambao wamefundishwa au kuelekezwa na mila na desturi zao kwamba, kabla hawajaoa, ni lazima wawe na nyumba kwanza, tena kwao. Kwa hiyo, hawa hadi waje wapate uwezo wa fedha wanakuwa wameshachelewa.

6 Kuna baadhi ya wanaume, maisha bila ya ndoa wanayaona kuwa ndiyo bora kuliko yale ya ndoa:
Kuna baadhi ya wanawake hujirahisisha sana kwa wanaume. Siku hizi ni jambo la kawaida sana kukuta mwanaume anaishi na mwanamke bila ndoa, wenyewe wanaita Trial Marriage. Na hapo ndipo unapokuta wanaume hawaoni tena umuhimu wa kuoa. Sasa kama mwanamke anaweza tu kuishi na mwanaume bila ya ndoa na mwanaume huyo akapata huduma zote kutoka kwa mwanamke huyo, unadhani ni kitu gani kitamvuta kufunga ndoa. Jambo lingine ni ile dhana kwamba maana ya ndoa ni tendo la ndoa. Siku hizi wanaume wengi wamejikuta wakiwa hawahitaji tena kuoa kwa sababu tendo hilo linapatikana kiurahisi tofauti na zamani. Siku hizi inawezekana kabisa kumtongoza binti leo na kupata tendo siku hiyo hiyo….. Na hapa siwazungumzii makahaba. Nawazungumzia mabinti zetu ambao wengine ukiwaona ni watu wa kuheshimiwa ukiwaangalia kwa nje lakini kwa ndani hawana lolote, vijana wa siku hizi wenyewe huwaita maharage ya Mbeya.

Kuna sababu nyingi zinazotajwa kusababisha wanaume siku hizi kujivuta sana katika kufanya maamuzi ya kutafuta mwenza. Lakini hizo chache nilizozitaja zina mchango mkubwa.

Aina Hii 10 Ya Wanawake Ambao Ukiwa Nao Watakuletea Matatizo ni Vyema Kuwaepuka

Japo kila mtu anakasoro zake ila kuna tabia ndogo ndogo ambazo huleta maharibiko kwenye mahusiano na kuufanya uhusiano kubadilika kutoka kwenye amani na utamu unaopaswa kuwa nao na kuwa mchungu iwapo mwanaume asipokuwa makini wakati wa uchaguzi wa mwenzi anaetaka kuwa nae.
Kiumeni.com tumejaribu kufanya utafiti na kuongea na wanaume walioachana na wenzi wao pamoja na wale waliopigwa chini japo wanang'ang'ania wao ndo waliowatema wapenzi wao na kuongea nao kwa mapana juu ya nini kiliwafanya wafikia uwamuzi huo mzito wa kuachana na wenzi wao, ndipo tukapata maelezo mengi na kukuandalia wewe mpenzi msomaji wa kiumeni.com aina ya wanawake kumi ambao inakubidi kufikilia mara mbili kwa marefu na mapana kabla ya uwamuzi wa kuamua kumpa sehemu ya maisha yako.

1. Mwanamke Mchungu: Unamjua yule mwanamke ambaye huwa na hasira na jinsia ya kiume muda wote? Huwa haishi kulalamika wanaume huwa ni wapumbavu, mwanaume haaminiki ni kama mbwa, yeye hasira yake huwa ipo juu ya wanaume muda wote na anaona mwanaume hawafai na hawana umuhimu wowote, hii inawezeka inatokea labda sababu ya katendwa na kuvunjwa moyo mara nyingi, mwanamke wa aina hii iwapo akiwekwa ndani huwa ni vurugu, kukosea inatokea ila kwake itakuwa ni matusi na kosa moja dogo atalichukulia kwa uzito wa ajabu ambao hata haupo, akiwa na hasira ni kutukana na kutoa maneno ya chuki na kashifa kutokana na kutendwa kwake nyuma na wanaume na mrundikano wa hisia ambazo hajazitatua moyoni mwake na hasira zake huwa ni za karibu maana anakuwa hamuamini mwanaume wake hivyo yupo tayari tayari kuangalia kosa ili apate sababu.

2. Mwanamke Mchoyo: Ukiwa unahitaji nyumba iwe na furaha na mwenza ambaye anahitaji furaha yako na ya kwake pia, unahitajika sana kukaa mbali na mwanamke mchoyo, mwanamke wa namna hii yeye huwa anakuwa anajiweka mbele tu kuangalia masilahi yake bila kuangalia hisia zako na tofauti na hapo hata ndugu zako wakija sababu ya ile choyo anasababisha mvurugano wa familia na siku zote huwezi kujikuta na furaha zaidi ya kuwaza kutatua tatizo hili kabla hujalimaliza limeingia jingine.

3. Mwanamke Mpenda vitu: mwanamke huyu la kwake pesa, hajakiona hiki anakitaka, kile nacho anataka bila kuangalia hali ya kiuchumi imekaaje, kamuona jirani Mama Naniii kavaa vile na yeye anataka ashindane nae, anakuwa anajari zaidi vitu vya kidunia bila kuangalia familia yake ipo katika hali gani, yupo radhi kuvunja familia, kuvunja uaminifu wake kwako na hata ule wa kidini ili tu hali ya kile anachokuwa anakihitaji moyoni kitimie. Na siku zote huwa hawezi kuwa mwenza mzuri zaidi ya kukuumiza kichwa na kupasua nyongo yako kwa mawazo ya kumridhisha pale ambapo hauna uwezo napo.

4. Mwanamke Mtongozwaji: Umevutika na yule mwanamke ambae yeye huwa na ukaribu na wanaume mmoja au mwingine kupitiliza? Anacheka cheka na mwanaume huyu na yule kama lile limjusi la kwenye mawe linahama kutoka jiwe moja kwenda jingine likitikisa kichwa kwa kujikubali bila kujishitukia na kufanya wanaume wengi wajihisi labda wanapendwa na msichana wako. Inakubidi uwe mwangalifu maana mwanamke wa hivi huwezi kumfanya mwenza wako maana iwapo hata ukimuoa tabia za namna hii huwa ni ngumu kuziondoa na atakuhisi labda unawivu unamfatilia sana sababu ameisha kaa sana nje ya msitari mpaka hajui mwisho wa mipaka ni wapi. Ukimuoa mwanamke huyu usije shangaa kusikia mkeo anasifa ya kujichekelesha kwa wanaume wa mtaa wako.

5. Mama Shughuli: Huyu ni shida, kila aina ya sherehe yeye kaalikwa na zote anaziudhuria, Diamond anaimba kwenye klabu ya karibu saa nane usiku yeye yupo, siku zote yeye anavaa nguo ya fasheni ya kisasa zaidi na ndo mkufunzi wa sherehe zijitokezazo, maisha yake yalishazoea hivyo na furaha yake na maongezi yake yanategemea hafla kubwa ijayo. Mwanamke wa sampuli hii huwa huwezi kumfanya mwenza na kuhisi utajenga nae familia, labda wewe ndo uwe mtunzaji watoto na mchunga nyumba wakati yeye yupo bize usiku na masherehe.

6. Mpenda kupewa kipaumbele: Japo ni jambo la kike kutaka kupewa kipaumbele na jamii, ila ukiwa ni ugonjwa hapa lazima jasho liwe linakutoka kila siku, mwanaume mzuri ni yule anaemjali mkewe, ila kama mke yeye ndo anataka umjali yeye tu, kila ukitaka utoke anataka akuone, hujaenda kibanda cha kuangalia mpira jirani ameshapiga simu urudi anashida na wewe, yeye anataka ya kwake tu bila kuangalia hata wewe unahitaji muda wako binafsi wa mambo mengine, ukiwa na mwenza wa namna hii unakuwa mtuma kwake badala ya kufurahia nawe maisha yako jinsi unavyozeeka polepole, kuishi kwako inakuwa ili umtimizie shida zake yeye.

7. Mwanamke Mbea: Je Saa zote yeye hana ya kwake, anataka kujua flani anaishije na anafanya nini?, mwanamke wa namna hii haumuhitaji. Manaume huitaji mwanamke ambae anauwezo wa kujenga familia na hii inaitaji akili ambayo inauezo a kutatua matatizo yanayoizunguka familia yake, kama mwanamke akili yake ipo bize kuaza Mama Majuto nyumba ya pili leo wamekula nini haezi kua na akili ya kujenga zaidi ya kuongeza umasikini ka kutumia muda wake kusema na kuongelea juu ya wengine badala ya kufanya kazi za kimaendeleo, na utakuwa na wakati mgumu pia wa kumfanya akufikilie kuhusu wewe, unafika nyumbani yeye yuko mtaa wa pili kaendea umbea.

8. Mwanamke Mwenye Deko: Kuna wanawake wengine wameshazoea kudekezwa kwao, na hana tabia ya kufanya kazi ili aweze kujitimizia mahitaji maana hajakuzwa hivyo na hii siku zote haipo kwenye sifa ya mwanamke mzuri na mke mzuri, hata kama ukijitoa na kujitahidi kumpa maisha aliyokwisha zoea, jua kabisa ukimuoa watoto lazima watatokea kwenye familia, na mama mwenye deko hawezi kukuza watoto maana watoto wanahitaji kazi kubwa ya kuwaangalia na kuwakuza. Hivyo mwanamke wa namna hii hatoweza kuwa mwenza mzuri.

9. Mwanamke Ambaye Hana Msimamo: Mwanamke ambae huwa na hali ngumu kufanya maamuzi ya chochote, (kikazi, kijamii, kirafiki, kimahusiano au kwa vyovyote vile..) na hivyo hivyo hatokuwa na uwezo kwenye maamuzi hasa kwenye ndoa, maana atakuwa bendela kifata upepo, mtu akimwambia hiki yeye atakiamini, kile vile vile atafuata huko huko, na itakuwa ngumu pia kuwa mke mzuri maana dunia imejaa maneno mengi na vishawishi vingi.

10. Mwanamke Mwenye Mdomo Mchafu: Je ukigombana naye kidogo maneno yake yanakuwaje? maneno ya kebehi hayamuhishi, akikasirika hata heshima baina yenu inakuwa haipo tena?, vipi kuhusu watu wengine anaowaona wapo chini ya hadhi yake?, Kama majibu unayojijibu yanaelekea hana heshima kwa binadamu wenzake basi hapo umekanyaga bomu, litalipuka muda wowote na iwapo likilipuka lazima litakuumiza kihisia, na iwapo ukimfanya akawa mkeo basi kaka lazima kila jioni baada ya kazi utapitia baa ilio kalibu nawe. Na kiumeni.com inaendelea kukupa pole kwa kuyapa shida maisha yako ambayo yangekuwa matamu zaidi iwapo ungegunduwa mapema

Wanawake Huvutiwa na Kitu Hiki kutoka kwa Mwanaume..Kama Huna Jitahidi Uwe Nacho


Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua. 

USAFI BINAFSI

Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Ni aghalabu sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi.

Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani.

Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.

KUJIAMINI

Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia manukato mapya!

Mathalani unakuwa naye katika mtoko, angependa kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.

Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na matege wala makengeza!

KUJITETEA

Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana na kilichopita, lakini hapa ni kwenye upande wa kujitetea zaidi. Wakati unapodai haki yako mbele ya mwanamke wako, suala la kujitetea linapewa nafasi kubwa sana.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi.

Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote!

Inapowezekana, uwe na uwezo wa ‘kuzichapa’ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.

Mwanaume aliye ‘fiti’ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.

KUJALI

Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali. Wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali.

Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai.

UKARIBU

Kati ya vitu vinavyowapa mshawasha mkubwa wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku.

Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi.

Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako. Hebu tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa!


KUMSIFIA

Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama ni jambo lisilo na maana sana kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda kuwasifia wanaume zao. Nitakupa mifano miwili ya namna wanandoa wa jinsia mbili tofauti wanavyotambulishana kwa jamaa zao. 

MWANAUME: “Peter kutana na mke wangu, anaitwa mama Diana. Nipo naye mwaka wa tatu sasa, tuna watoto wawili, huyo Diana na mwingine anaitwa Cris. Mama Diana, huyu ni Peter nilisoma naye A – Level, Tosamaganga Sekondari.”

MWANAMKE: “Suzan, huyu ndiye mume wangu mpenzi...anaitwa Elifaraja lakini mimi napenda zaidi kumuita Elly. Kiukweli nampenda sana mume wangu jamani, tuna mtoto wetu mmoja, anaitwa Agness. (Akimgeukia mumewe) Baby, huyu hapa ni rafiki yangu Suzan. Yaani tumekua naye mtaa mmoja huko Arusha.”

ANGALIA TOFAUTI

Bila shaka kwa namna wawili hao walivyotambulishana unaweza kuona tofauti kubwa. Mwanaume amemtambulisha mkewe kawaida kabisa, hajaonesha manjonjo au namna anavyompenda na kumthamini mwenzake, lakini mwanamke amefanya hivyo.

Sikia nikuambie, KUMSIFIA mwanamke, kuna nafasi kubwa sana kwake. Chunguza kwa makini, hata kunapokuwa na mgongano katika familia, halafu wakatokea wageni, baada ya utambulisho na mazungumzo ya hapa na pale, wageni wakiondoka kunakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kumaliza mpasuko katika familia.

Jenga utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, unamuweka katika kilele cha upendo. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye.

MALENGO

Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwa siri na wakati mwingine ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa mshtukizo baada ya kukamilisha jambo husika.

Hii si sahihi. Dunia ya leo imebadilika rafiki zangu. Inawezekana wazee wa zamani walikuwa sahihi, maana ilikuwa ni suala la kununua ng’ombe na kuwaweka katika zizi kwenye kijiji cha jirani, halafu wanapewa malisho mazuri, baada ya miaka miwili wanazaliana, hapo ndipo anamweleza mkewe.

Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo mengi. Kuna suala la hasara katika biashara, utapeli n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa kuliko wote, ndiye ndugu yako wa karibu zaidi kuliko yeyote. Yes! Mkeo ndiye ndugu yako maana umetengeneza naye familia. Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga maisha pamoja.
Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.

Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu.

KIPAUMBELE

Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mkeo akawa katika hali hiyo, msikilize.

Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumani kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa ada shuleni’.

Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia, mshirikishe.

Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.

TENDO LA NDOA 

Hiki ni kipengele nyeti, kinachohitaji lugha nzuri ya kirafiki kukifafanua. Hakuna siri, tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi cha ndoa. Maana hata maandiko yanasema: “Mwanamke ataacha wazazi wake na kwenda kwa mumewe, nao watakuwa mwili mmoja.”

Kimsingi tendo la ndoa lina nafasi yake. Ni muhimu likaheshimiwa na kutengewa muda maalum wa kufurahia. Si papara. Kwa bahati mbaya wanaume huwa si wafuatiliaji sana wa kujua namna ya kuwafurahisha zaidi wenzao. Wenyewe wanajiwazia wenyewe. Wanafikiria namna ya kuwakomoa wenzao.
Si sahihi. 

Tendo la ndoa halina maana ya kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza hisia za mwenzako. Ukiweza kumjulia mke wako katika eneo hili, ni wazi kwamba utazidisha upendo wake kwako, lakini pia atakuwa katika kuta za uaminifu. Akatafute nini nje wakati wewe ndiye mganga wake unayeweza kumtibu barabara?

Kuna kitu nimesahau kweli? Kama kipo nitafute pembeni, kwa hapa haya yatoshe kukufanya uelewe nilichotaka kukuelekeza. Nikuache na neno moja; uamuzi wa kuijenga ndoa yako upo mikononi mwako. Ukitaka iwe shaghalabaghala, pia ni wewe tu!

Mh.Nape Afunguka Haya Kuhusu Serikali ya Rais Magufuli


Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema ataendelea kuwa mtiifu kwa Rais John Magufuli, Serikali na Chama cha Mapinduzi tofauti na maneno yanayosemwa mitandaoni.

Tangu alipoachwa kwenye mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, Machi 23, kumekuwa na taarifa nyingi feki kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuenguliwa kwake zikidaiwa kutolewa na mbunge huyo wa Mtama ambazo hata hivyo, amekuwa akizikanusha.

Akizungumza jana wakati akikabidhi ofisi kwa waziri mpya wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe katika ofisi za wizara hiyo mjini hapa, bila kutaja maneno hayo ya mitandaoni, Nape alisema ataendelea kumuunga mkono Rais katika dhamira yake njema ya kuleta mageuzi nchini.

“Heshima aliyonipa Rais ni kubwa mno na nitaendelea kumuunga mkono katika dhamira yake njema ya kuleta mageuzi nchini” alisema.

Alimshukuru Rais kwa kumpa dhamana ya kusimamia wizara hiyo kwa miezi 15 baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya kwanza. “Nitaendelea kutoa ushirikiano kwa wizara hii kwa sababu mimi ni mdau mkubwa wa sekta hiyo,” alisema.

Waziri Mwakyembe alisema ataendeleza mazuri yote yaliyofanywa na Nape katika kuimarisha wizara hiyo na atahakikisha wizara hiyo inakuwa ya mfano nchini.

Alimsifu Nape akisema katika kipindi kifupi alichokaa katika wizara hiyo amefanya mabadiliko na watu wameanza kuifahamu.

Nape aliondolewa katika nafasi hiyo siku moja baada ya kamati aliyounda kuchunguza tukio la kuvamiwa kwa ofisi za Clouds kumkabidhi ripoti.

Mara baada ya kupewa ripoti hiyo, Nape aliahidi kuikabidhi kwa mamlaka zake za juu akizitaja kuwa ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais lakini asubuhi ya siku iliyofuata aliondolewa katika nafasi hiyo.

Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na viongozi wengine wa wizara hiyo, naibu waziri, Anastazia Wambura, katibu mkuu, Profesa Elisante Ole Gabriel na naibu katibu mkuu, Nuru Millao.